Thursday, August 20, 2015

AMANI MEYA WA BUKOBA ANYIMWA FOMU YA KUGOMBEA UDIWANI BUKOBA






MSIMAMIZI   wa   uchaguzi  Kata  ya Kagondo   Sharifa  Mstafa,   amnyima  fomu  mgombea  udiwani wa Kata hiyo   aliyekuwa Meya  wa Manispaa ya Bukoba Anatory Amani,  kupitia tiketi ya chama cha (NCCR-MAGEUZI ) kwa  madai  ya kupokea maelekezo  kutoka  kwa msimamizi  wa Jimbo la Bukoba Mjini.


Mstafa,alisema sababu ya kukataa kutoa fomu kumesababishwa na kupokea barua mbili kutoka chama hicho moja ikitoka ofisi ya chama cha ( NCCR-MAGEUZI )Mkoa wa Kagera na nyingine kutoka wilayani zikiwa  na maelekezo tofauti.



Alisema barua iliyotoka ofisi ya Mkoa ya chama hicho iliyoandikwa tarehe 18/08/2015  saa  9.58 Alasiri  yenye kumbukumbu NA.NCCR- MAGEUZI/MM/KU/VOL.11/14/03 iliyosainiwa na kamishna wa  chama  hicho mkoa wa Kagera Peterson Mganyizi  ikimtambulisha Anatory Amani kuwa mteuliwa wa kugombea udiwani wa chama hicho na kuwa watampeleka kuchukua fomu Agost 19 mwaka huu.



Aliongeza   kuwa Agosti 19 mwaka  huu majira ya saa 2:3asubuhi alipokea barua kutoka chama hicho ngazi ya Wilaya ikimueleza kuwa chama hicho hakina mgombea wa udiwani Kata ya Kagondo.

WALENGWA KAYA MASKINI WAANZA KUPOKEA PESA ZA TASAF AWAMU YA TATU KARAGWE


Na  Juhudi  Felix-Karagwe

Mkuu  wa    wilaya  ya  Karagwe  Deodatus    Kinawiro  amezindua  rasmi    shughuli  ya  uhawilishaji  fedha  za  mpango  wa  kunusuru  Kaya  maskini  zipatazo  9,810  katika  halimashauri  ya  wilaya  ya  Karagwe  ambazo  zitagharimu  kiasi  cha  shilingi 370,568,000    zilizotolewa  kwa  walengwa  kwa  awamu   ya  kwanza.
Uzinduzi  huo  ulifanyika  jana  katika  kijiji  cha  Bisheshe   Kata  ya  Nyakahanga  wilaya  ya  Karagwe  ambapo  mkuu  wa  wilaya  ya  Karagwe  aliwataka  walengwa  wa  mradi  huo  ambao  unasimamiwa  na   Mfuko  wa  Maendeleo  ya  Jamii  yaani  TASAF    lengo  lake  likiwa  ni   kuzinusuru  Kaya  Masikini  nchini  Tanzania  lazima wataalamu  wahakikishe  walengwa  wote  wa  mradi  huo  wanapata  haki  yao  ya  msingi.

Alisema  TASAF  awamu ya  tatu  ni  utekelezaji  wa  Ilani  ya  CCM  ambayo  ilitumia  kauli  mbiu  ya  maisha  bora  kwa  kila  mtanzania  hivyo  katika  kutekeleza  hivyo  wanasaidia  kupunguza  ukali  wa  maisha  kwa  kuanzisha  miradi  mbalimbali  akitolea  mifano  ya  ujenzi  wa  shule  za  sekondari  kila  kata,ujenzi  wa  zahanati  na  vituo  vya  afya  na  miradi  mingineyo  ambayo  inalenga  kusongeza  huduma  kwa  wananchi.

Maria   Aloyce  miaka  (63)mtu  anayeishi  na  ulemavu  wa  viungo  alisema  pesa  za  mradi  wa  TASAF  alizozipokea  zitamsaidia  kununulia  daftari  wajukuu  wake  watatu   ambao  kwa  sasa  wanamtegemea  na kusema  kuwa  ni  faraja  maana  kutokana  na  hali  yake  aliyonayo  alikuwa  hana  usaidizi  wa  kutimiza   mahitaji   yake  kama  inavyotakiwa.



Mlengwa  mwingine   aliyeongea  na  waandishi  wa  habari  ni  Ngalinda  Stansilaus (12)anayesoma  darasa  la  tano  katika  shule  ya  msingi  Bisheshe  alisema  pesa  hiyo  ya  mradi  wa  TASAF  itamsaidia  katika  kununua  daftari,sare  za  shule  na  itakayosalia  ataitumia  kwa  kununua  mahitaji  ya  nyumbani  maana  baba  yake   Stansilaus  Masoud miaka (72)ni  mgonjwa  alipooza  miaka  5  sasa hivyo  hana  usaidizi  wowote  na  anaishi  naye  nyumbani  na  husaidiwa  na  majirani  anapokuwa  shule.

Hata  hivyo  walengwa  hao  wa  TASAF  awamu  ya  tatu  walinungunikia  kitendo  cha  Mkuu  wa  wilaya  ya  Karagwe Deodatus  Kinawiro  kufika  kwenye  uzinduzi  huo   akiwa  ameambatana  na  Katibu  msaidizi  wa  CCM wilaya  ya  Karagwe  Denis  Mwita  akiwa  amevalia  mavazi  ya  chama  hicho  wakisema  huo  haukuwa  mkutano  wa  Kampeni  na  mradi  huo  siyo  wa  chama ni  kwa  watanzania  wote.

WALIMU 47 WA AJIRA MPYA WAINGIA MITINI

WALIMU 47 wa shule za sekondari kati ya 133,  waliokuwa wamepangwa na serikali kwenye ajira mpya mwaka huu, kwenye halmashauri ya wilaya ya Bukoba mkoani Kagera bado hawajaripoti  katika Vituo vyao vya kazi.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Graides Dyamvunye alisema kuwa mpaka sasa ni walimu 86, ambao tayari  wameripoti kwenye Vituo vyao vya kazi wakiendelea na shughuli zao za ufundishaji.

Alisema tarehe ya mwisho ya kuripoti kwa walimu hao, katika vituo vyao vya kazi ilikuwa Juni 9 mwaka huu na kusisitiza kuwa matumaini ya walimu hao kuripoti ni mdogo kutokana na muda wa kuripoti kuisha bila kuwepo kwa taarifa zao.

Wednesday, August 19, 2015

watoto 300,000 huzaliwa na ugonjwa wa Selimundu





WATOTO laki 3 wa Afrika  huzaliwa wakiwa na ugonjwa wa seli mundu kwa mwaka .

Takwimu hizo zilitolewa na Dk. Digna Riwa  bingwa  wa magonjwa  ya  ndani kutoka hospitali ya Amana Jijini Dar-es-Salaam wakati wa kampeni ya magonjwa yasiyoambukiza iliyofanyika mkoani Kagera  hivi majuzi.

Riwa alisema  kutokana na utafiti wa wataalam  kutoka  katika hospitali ya Rufaa ya Muhimbili  umebainisha hari hiyo.

WANAOTUMIA VYANDARUA KUVULIA SAMAKI KUSHITAKIWA





SERIKALI mkoani Kagera imewaaagiza watendaji  wa kata na mitaa Mkoani humo kusimamia kikamilifu zoezi la ugawaji wa vyandarua ikiwa sambamba na  kuwakamata wale wote watakaotumia vyandarua hivyo kwa kuzungushia katika bustani, vibanda vya kuku pamoja na kuvulia samaki.



Kauri hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa mkoa wa Kagera John Mongella wakati wa akizindua zoezi la  kugawa vyandarua ililiofanyika jana wilayani ya Bukoba.



Mongella alisema kuwa kumekuwepo na tabia ya watu kushindwa kutambua matumizi sahihi ya neti na badara yake wanatumia katika uvuvi na ufugaji kitu ambacho si sahihi.