Thursday, August 20, 2015

AMANI MEYA WA BUKOBA ANYIMWA FOMU YA KUGOMBEA UDIWANI BUKOBA






MSIMAMIZI   wa   uchaguzi  Kata  ya Kagondo   Sharifa  Mstafa,   amnyima  fomu  mgombea  udiwani wa Kata hiyo   aliyekuwa Meya  wa Manispaa ya Bukoba Anatory Amani,  kupitia tiketi ya chama cha (NCCR-MAGEUZI ) kwa  madai  ya kupokea maelekezo  kutoka  kwa msimamizi  wa Jimbo la Bukoba Mjini.


Mstafa,alisema sababu ya kukataa kutoa fomu kumesababishwa na kupokea barua mbili kutoka chama hicho moja ikitoka ofisi ya chama cha ( NCCR-MAGEUZI )Mkoa wa Kagera na nyingine kutoka wilayani zikiwa  na maelekezo tofauti.



Alisema barua iliyotoka ofisi ya Mkoa ya chama hicho iliyoandikwa tarehe 18/08/2015  saa  9.58 Alasiri  yenye kumbukumbu NA.NCCR- MAGEUZI/MM/KU/VOL.11/14/03 iliyosainiwa na kamishna wa  chama  hicho mkoa wa Kagera Peterson Mganyizi  ikimtambulisha Anatory Amani kuwa mteuliwa wa kugombea udiwani wa chama hicho na kuwa watampeleka kuchukua fomu Agost 19 mwaka huu.



Aliongeza   kuwa Agosti 19 mwaka  huu majira ya saa 2:3asubuhi alipokea barua kutoka chama hicho ngazi ya Wilaya ikimueleza kuwa chama hicho hakina mgombea wa udiwani Kata ya Kagondo.

No comments:

Post a Comment