Na
Juhudi Felix-Karagwe
Mkuu wa wilaya
ya Karagwe Deodatus
Kinawiro amezindua rasmi
shughuli ya uhawilishaji
fedha za mpango
wa kunusuru Kaya
maskini zipatazo 9,810
katika halimashauri ya
wilaya ya Karagwe
ambazo zitagharimu kiasi
cha shilingi 370,568,000 zilizotolewa kwa
walengwa kwa awamu
ya kwanza.
Uzinduzi
huo ulifanyika jana katika kijiji
cha Bisheshe Kata
ya Nyakahanga wilaya
ya Karagwe ambapo
mkuu wa wilaya
ya Karagwe aliwataka
walengwa wa mradi
huo ambao unasimamiwa
na Mfuko wa
Maendeleo ya Jamii
yaani TASAF lengo
lake likiwa ni
kuzinusuru Kaya Masikini
nchini Tanzania lazima wataalamu wahakikishe
walengwa wote wa
mradi huo wanapata
haki yao ya
msingi.
Alisema
TASAF awamu ya tatu
ni utekelezaji wa
Ilani ya CCM
ambayo ilitumia kauli
mbiu ya maisha
bora kwa kila
mtanzania hivyo katika
kutekeleza hivyo wanasaidia
kupunguza ukali wa
maisha kwa kuanzisha
miradi mbalimbali akitolea
mifano ya ujenzi
wa shule za
sekondari kila kata,ujenzi
wa zahanati na
vituo vya afya
na miradi mingineyo
ambayo inalenga kusongeza
huduma kwa wananchi.
Maria
Aloyce miaka (63)mtu
anayeishi na ulemavu
wa viungo alisema
pesa za mradi
wa TASAF alizozipokea
zitamsaidia kununulia daftari
wajukuu wake watatu
ambao kwa sasa
wanamtegemea na kusema kuwa
ni faraja maana
kutokana na hali
yake aliyonayo alikuwa
hana usaidizi wa
kutimiza mahitaji yake
kama inavyotakiwa.
Mlengwa mwingine aliyeongea
na waandishi wa
habari ni Ngalinda
Stansilaus (12)anayesoma
darasa la tano
katika shule ya
msingi Bisheshe alisema
pesa hiyo ya
mradi wa TASAF
itamsaidia katika kununua
daftari,sare za shule
na itakayosalia ataitumia
kwa kununua mahitaji
ya nyumbani maana
baba yake Stansilaus
Masoud miaka (72)ni mgonjwa alipooza
miaka 5 sasa hivyo
hana usaidizi wowote
na anaishi naye
nyumbani na husaidiwa
na majirani anapokuwa
shule.
Hata
hivyo walengwa hao
wa TASAF awamu
ya tatu walinungunikia kitendo
cha Mkuu wa
wilaya ya Karagwe Deodatus Kinawiro
kufika kwenye uzinduzi
huo akiwa ameambatana
na Katibu msaidizi
wa CCM wilaya ya
Karagwe Denis Mwita
akiwa amevalia mavazi
ya chama hicho
wakisema huo haukuwa
mkutano wa Kampeni
na mradi huo
siyo wa chama ni
kwa watanzania wote.
No comments:
Post a Comment