Monday, April 18, 2016

Tanzania claimed MCC Board

President Magufuli said he did not want bilateral aid complies with the conditions, titled 'bread mocking'. He stressed that Victor is your victory is better than eating cassava bread.

He stated this yesterday when he laid the foundation stone for the construction of the first road to the top (flyover), creates an intersection of Mandela and Nyerere area TAZARA Dar es Salaam. The road to the top is being built with funding from the Government of Japan. We congratulate the President for his statement that Magufuli about aid donor countries.

We say this because this is the first time for President Magufuli discuss aid from the Millennium Challenge Corporation (MCC) of the United States, to withdraw support to the Government of Tanzania to US $ 472.8 million equivalent to almost one trillion shillings.

MCC halted such assistance on the grounds that the government has not taken steps to respect freedom of expression and freedom of association in the implementation of the Law of Criminal Network and also that the government did not take action regarding the choice of destination of Zanzibar, held on March 20, this year.

Tanzania claimed MCC Board continued with the choice of destination, which is to share with you all and not all ukuakisi opinion, despite complaints from the US government and the international community. These decisions should not have given to MCC, based on good relationships and long term between the United States and Tanzania.

These two nations have been collaborating in various fields, eg education and health for many years. MCC was necessary to be done and was continuing to talk with the government of Tanzania on those two issues and get clarification; instead of taking a sudden decision to suspend aid.

In addition, we are backed President Magufuli for his statement about the Government of Japan, that Japan is a true friend of Tanzania, as has been giving aid without conditions or threats, eg assistance building many roads in the country. Japanese Finance made it to their taxpayers.

For example in road construction that top constructed in areas set of TAZARA, Japan has provided money to taxpayers his billion shillings 93.44 and Tanzania has provided Sh 8.3 billion to make the project costing more than Sh 100 billion Generally speaking, we thank the very government of Japan and citizens his influences how the various projects of Tanzania.

We know most of the world countries are friends and Tanzania continued to have a relationship with them for many years. So we appeal to them with, follow the example of Japan to provide aid without conditions.

And if you had provided unconditional aid to Tanzania, then continue to do so. We remind donors that Tanzania does not need donors, who give aid and conditional alarming. Better than eating cassava bread kusimangwa.

Friday, August 21, 2015

AJINYONGA BAADA YA KUKATALIWA NA MCHUMBA WAKE AMBAYE WALIKUWA WAFUNGE NDOA 28.08.2015


Na Juhudi  Felix-KYERWA

Mtu mmoja  mkazi  wa  Kitongoji cha  Kishanda B Kijiji cha Kyerwa   Kata  ya  Kyerwa  wilayani  Kyerwa  mkoani  Kagera  amekutwa amejinyonga  nyumbani  kwake  na  kuacha  ujumbe unaelezea sababu  za  kujinyonga  kwake   kuwa  ni  kukataliwa kwa  mchumba  wake  waliokuwa  wanatarajia  kufunga  ndoa  Agosti 28  mwaka  huu.

Akithibitisha tukio  hilo  jana  mwenyekiti  wa  kitongoji hicho Ibrahimu  Paschal alisema  kuwa  aliyejinyonga  ni Sabinus  Gabriel  miaka (30) na alitumia  kamba  ya  katani  aliyoifunga  kwenye  dari    ya  nyumba  yake.

Alisema  marehemu  aliacha  ujumbe aliouandika  ukielezea   sababu  zilizopelekea  kuchukua  uamuzi  huo  wa  kujiua  kuwa  ulitokana  na  kukataliwa  na  binti  aliyekuwa  anamchumbia  na  taratibu  zilikuwa  zimeishakamilika  na  mchumba  wake  huyo  kubadili  maamuzi  ghafla  na  kumweleza  hamtaki  tena  kwasababu  amempata  mwingine.

Aliyejinyonga  alitarajia  kufunga  ndoa  Agosti 28  mwaka  huu  ambapo  wana  ndugu  walieleza  kuwa  taratibu  za  kutoa  mahali  zilikuwa  zimeishafuatwa  ambapo  Jumatatu  ya  Agosti 17  mwaka  huu  baadhi  ya  vitu  vilipelekwa  kwa  wazazi  wake  na  binti.




Mwenyekiti  huyo  alisema  kuwa  tukio  hilo  la  watu  kujinyonga  katika  kijiji  hicho  ni  la  pili  ndani  ya  wiki  mbili  kwani  kuna  baba   mmoja alijinyonga  baada  ya  mke  wake  kuondoka  na  kurudi  kwa  wazazi  wake  huku  akihaidi  kutorudi   kwake  na  ndoa  yao  haipo  tena  kutokana  na  kile  kilichodaiwa  ni  kuwepo  migogoro  ya  muda  mrefu ndani  ya  familia  hiyo.

Aidha  Mzazi wa marehemu Gabriel  Rubinduka  alieleza kusikitishwa na tukio  la  kifo cha mtoto wake ambaye walitarajia kumfanyia sherehe  kama walivyokuwa wameazimia kutokana na maandalizi yaliyokuwa yamefanyika katika familia yao.

“Ni majonzi  makubwa  kweli  familia  tulishajiandaa  kumwandalia  sherehe  kubwa  lakini  hili lililomtokea  sijui  kama  ni  mipango  ya  Mungu  ila  yote  tunamwachia  aliyetuumba  na  kilichobakia  ni  kuendelea  kumwombea  pumziko  la  Amani”Alisema  Gabriel
Binti  aliyekuwa  anachumbiwa  Jovitha  Novath   alipofuatwa  na  waandishi wa  habari  kuelezea   mkasa  huo  kama  ujumbe  ulioachwa  na  marehemu  kama  una  ukweli  ndani  yake  hakuwa   tayari  kuzungumzia  tukio  hilo.

Kwa  upande  wake  Novath  Kalekona  ambaye  ni  mzazi  wa  binti  aliyekuwa  anachumbiwa  alikiri  kuwa  ni  kweli  binti  yake  kuchumbiwa  na  huyo  aliyejinyonga  na  kusema  kuwa  ni kweli  baadhi ya  mali  alikwishapokea  kutoka  kwa  wazazi  wake  na  marehemu.

“Ni  kweli   wazazi  wa  marehemu  walileta  mali  ambazo  kwa  makubaliano  ambayo  ni  taratibu  ambazo  ni  utamaduni  wetu  lazima  kuzitimiza  na  walikuwa  kwangu  jumatatu  ya  Agosti 17  mwaka  huu  lakini  hili  la  kujinyonga  limenishutua  hata  mimi na  hatukujua kama  kuna  hali  kama  hiyo  maana  walikuwa  wakipendana  kweli”Alisema  Kalekona

Jeshi  la  polisi  wilayani  Kyerwa  wameruhusu  mwili  wa  marehemu  kuzikwa  baada  ya  uchunguzi  wa  kitabibu  uliofanywa  na  mganga mfawidhi   kutoka  Zahanati  ya  Kimuli Braisoni  Katabaro.

AWUWAWA NA KUCHOMWA MOTO BAADA YA YEYE NAYE KUMUUA MAMA YAKE WA KAMBO


Na  Juhudi   Felix- KYERWA

Matukio  ya  wananchi  kujichukulia  sheria  mikononi  na  kuwapiga,kuwachoma  moto watuhumiwa  wanaowakamata  yanazidi  kuongezeka  wilaya  ya   Kyerwa  na  Karagwe  mkoani  Kagera  baada ya  wananchi  wa Kitongoji  cha  Nyabihara kijiji  cha  Kibingo  kata  Kibingo  kupinga  kisha  kumchoma  kwa  moto   kijana  mmoja  aliyetambuliwa  kwa  jina  la Thomas  Tumuhirwe miaka (24) baada  ya  yeye  kumua  mama  yake  wa  Kambo Juliana  Tumuhirwe  miaka (57)

 Akithibitisha  kutokea  tukio  hilo  jana  afisa mtendaji wa kata ya Kibingo   Geofrey Mihambwe alisema tukio hilo limetokea  usiku wa Agosti 19 mwaka huu ambapo kijana huyo ambaye kwa sasa ni  Marehemu alimuua Mama  yake  huyo  kwa kumkata na panga sehemu ya shingo pia kumchoma kisu kifuani  juu  ya  titi  la  kushoto.

Alisema  kuwa chanzo cha mauaji hayo kimetokana na visa vilivyokuwepo baina ya hao marehemu na kuwa siku za nyuma  kijana  huyo  Thomasi  Tumuhirwe  aliwahi  kuhukumiwa kifungo  jela kufuatia kumuibia mama huyo  mbuzi  wake  watano.


Wananchi  walioongea  na  waandishi  wa  habari   katika  eneo  la  tukio  walisema  kijana  huyo  aliyeuwawa  kisha  kuchomwa moto  alikuwa  akijihusisha  na  vitendo  vya  wizi  wa  mali  kwenye  kijiji  hicho.

Rutambi  Mabati  alisema  kuwa   kutokana  na  tabia  hizo  wananchi   ndiyo  maana  waliamua  kuchukua  hatua  hiyo  ili kukomesha  wizi  na  vitendo  vya  kijana  huyo.

Marehemu  mama  Juliana  Tumuhirwe miaka (57), hakubahatika  kupata  mtoto  katika    maisha  yake kwani  majirani  walieleza  kuwa  alikuwa  akijufungua  watoto  kisha  wanafariki  dunia.

Polisi  wilayani Kyerwa limethibitisha kutokea kwa vifo hivyo ambapo mganga mfawidhi kutoka zahanati ya Kibingo Diana Tamba alifika eneo la tukio na kufanya uchunguzi wa kitababu kisha kuruhusu miili ya marehemu  kuzikwa.

Hata hivyo polisi wamewataka wananchi kutojichukulia sheria mkononi kuwa  hakuna mwananchi akiye juu ya sheria na kuwaasa kutii sheria bila shurti.

VIJANA WANAOJIITA VIBARU KATIKA MRADI WA REA WAGOMBA KUFANYA KAZI KISHA MALIPO YAO.


Na Juhudi   Felix-KARAGWE.

Vijana wanaofanya kazi katika mradi wa umeme vijijini (REA) katika  laini  ya Nkwenda wamegoma kufanya kazi kwa siku ya leo agosti 21 kisha kuzingira ofisi za Rea zilizopo Wilayani Karagwe kwa madai ya kutolipwa malipo yao kwa muda mrefu.

 Vijana hao ambao wameeleza kuwa shughuli yao ni kuchimba mashimbo na kutandaza nyaya za umeme wamefikia hatua hiyo baada ya kutolipwa malipo yao kwa muda wa wiki tano.

Wameeleza kuwa makubaliano ya kazi hiyo ni kulipwa kila baada ya wiki moja lakini makubaliano hayo yamevunjwa na kuwasababishia kuishi kwa kutangatanga kwani hawana pesa ya kujikimu.

Vijana hao wameeleza kuwa endapo ofisi za REA zitashindwa kuwapatia madai yao watahakikisha wanaharibu nguzo ambazo walikuwa wamekwisha kuzijenga kutokana na kuwa hawajatendewa haki zao za msingi.

Mhandisi wa REA wilayani Karagwe Baraka Marco amewataka vijana hao kuwa na subira na  muda wowote watalipwa madai yao ambayo wanadai kwani mipango ya kuwalipa pesa yao inaendelea.

SHAHIDI WA NNE KATIKA KESI YA ALIYEKUWA MEYA WA MANISPAA YA BUKOBA AKAMILISHA USHAHIDI WAKE


SHAHIDI wa nne kwa upande wa utetezi, katika kesi ya aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Bukoba  Anatory Amani, amekamilisha kutoa ushahidi wake, baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Kagera kukubali kupokea CD mbili kama Vielelezo vya ushahidi wake.

Katika kesi hiyo ya Madai Namba mbili ya mwaka 2014,  Amani anaiomba  Mahakama hiyo imwamrishe Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba,  amfungulie  Ofisi  na kumtimizia haki zake kama Meya wa Manispaa hiyo.

Katika Vielelezo hivyo, Shahidi huyo ambaye ni Afisa Habari wa mkoa wa Kagera, Silyvestar Raphael alitoa CD mbili moja na Video na nyingine ya Sauti za mkutano ulioitishwa kwa ajili ya kusoma taarifa za ukaguzi maalumu uliofanywa na CAG- katika manispaa ya Bukoba.


Agost 10 mwaka huu, shahidi huyo hakumaliza kutoa ushahidi wake, baada ya kuibuka mabishano ya kisheria kati ya mawakili wa serikali wanaosimamia kesi hiyo na Wakili wa malalamikaji Aron Kabunga juu ya kupokea au kutopokea Vielelezo hiyo.

Thursday, August 20, 2015

KAYA 59667 KUNUFAIKA NA MPANGO WA TASAF AWAMU YA TATU KAGERA









Picha ya kwanza nai mkuu wa Wilaya ya Bukoba Jackson Msome aliyevaa suti akitoa pesa kwa Mariam Mussa mmoja wa wananchi waishio katika mazingira magumu kutoka Bukoba vijijini kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Kagera John Mongella


Picha ya Pili ni  baadhi ya wananchi waishio katika kaya maskini walioudhulia uzinduzi wa mpango huo.


Mkoa wa Kagera wazindua TASAF awamu ya tatu kwa lengo likiwa ni  kunusuru kaya maskini  ambapo kaya 59667 zategemewa kunufaika na mpango huo.

AMANI MEYA WA BUKOBA ANYIMWA FOMU YA KUGOMBEA UDIWANI BUKOBA






MSIMAMIZI   wa   uchaguzi  Kata  ya Kagondo   Sharifa  Mstafa,   amnyima  fomu  mgombea  udiwani wa Kata hiyo   aliyekuwa Meya  wa Manispaa ya Bukoba Anatory Amani,  kupitia tiketi ya chama cha (NCCR-MAGEUZI ) kwa  madai  ya kupokea maelekezo  kutoka  kwa msimamizi  wa Jimbo la Bukoba Mjini.


Mstafa,alisema sababu ya kukataa kutoa fomu kumesababishwa na kupokea barua mbili kutoka chama hicho moja ikitoka ofisi ya chama cha ( NCCR-MAGEUZI )Mkoa wa Kagera na nyingine kutoka wilayani zikiwa  na maelekezo tofauti.



Alisema barua iliyotoka ofisi ya Mkoa ya chama hicho iliyoandikwa tarehe 18/08/2015  saa  9.58 Alasiri  yenye kumbukumbu NA.NCCR- MAGEUZI/MM/KU/VOL.11/14/03 iliyosainiwa na kamishna wa  chama  hicho mkoa wa Kagera Peterson Mganyizi  ikimtambulisha Anatory Amani kuwa mteuliwa wa kugombea udiwani wa chama hicho na kuwa watampeleka kuchukua fomu Agost 19 mwaka huu.



Aliongeza   kuwa Agosti 19 mwaka  huu majira ya saa 2:3asubuhi alipokea barua kutoka chama hicho ngazi ya Wilaya ikimueleza kuwa chama hicho hakina mgombea wa udiwani Kata ya Kagondo.