Na Juhudi
Felix-KARAGWE.
Vijana wanaofanya kazi katika mradi wa umeme vijijini
(REA) katika laini ya Nkwenda wamegoma
kufanya kazi kwa siku ya leo agosti 21 kisha kuzingira ofisi za Rea zilizopo
Wilayani Karagwe kwa madai ya kutolipwa malipo yao kwa muda mrefu.
Vijana hao
ambao wameeleza kuwa shughuli yao ni kuchimba mashimbo na kutandaza nyaya za
umeme wamefikia hatua hiyo baada ya kutolipwa malipo yao kwa muda wa wiki tano.
Wameeleza kuwa makubaliano ya kazi hiyo ni kulipwa
kila baada ya wiki moja lakini makubaliano hayo yamevunjwa na kuwasababishia
kuishi kwa kutangatanga kwani hawana pesa ya kujikimu.
Vijana hao wameeleza kuwa endapo ofisi za REA
zitashindwa kuwapatia madai yao watahakikisha wanaharibu nguzo ambazo walikuwa
wamekwisha kuzijenga kutokana na kuwa hawajatendewa haki zao za msingi.
Mhandisi wa REA wilayani Karagwe Baraka Marco
amewataka vijana hao kuwa na subira na muda wowote watalipwa madai
yao ambayo wanadai kwani mipango ya kuwalipa pesa yao inaendelea.
No comments:
Post a Comment