Wednesday, August 19, 2015

WANAOTUMIA VYANDARUA KUVULIA SAMAKI KUSHITAKIWA





SERIKALI mkoani Kagera imewaaagiza watendaji  wa kata na mitaa Mkoani humo kusimamia kikamilifu zoezi la ugawaji wa vyandarua ikiwa sambamba na  kuwakamata wale wote watakaotumia vyandarua hivyo kwa kuzungushia katika bustani, vibanda vya kuku pamoja na kuvulia samaki.



Kauri hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa mkoa wa Kagera John Mongella wakati wa akizindua zoezi la  kugawa vyandarua ililiofanyika jana wilayani ya Bukoba.



Mongella alisema kuwa kumekuwepo na tabia ya watu kushindwa kutambua matumizi sahihi ya neti na badara yake wanatumia katika uvuvi na ufugaji kitu ambacho si sahihi.

No comments:

Post a Comment