Friday, August 21, 2015

AWUWAWA NA KUCHOMWA MOTO BAADA YA YEYE NAYE KUMUUA MAMA YAKE WA KAMBO


Na  Juhudi   Felix- KYERWA

Matukio  ya  wananchi  kujichukulia  sheria  mikononi  na  kuwapiga,kuwachoma  moto watuhumiwa  wanaowakamata  yanazidi  kuongezeka  wilaya  ya   Kyerwa  na  Karagwe  mkoani  Kagera  baada ya  wananchi  wa Kitongoji  cha  Nyabihara kijiji  cha  Kibingo  kata  Kibingo  kupinga  kisha  kumchoma  kwa  moto   kijana  mmoja  aliyetambuliwa  kwa  jina  la Thomas  Tumuhirwe miaka (24) baada  ya  yeye  kumua  mama  yake  wa  Kambo Juliana  Tumuhirwe  miaka (57)

 Akithibitisha  kutokea  tukio  hilo  jana  afisa mtendaji wa kata ya Kibingo   Geofrey Mihambwe alisema tukio hilo limetokea  usiku wa Agosti 19 mwaka huu ambapo kijana huyo ambaye kwa sasa ni  Marehemu alimuua Mama  yake  huyo  kwa kumkata na panga sehemu ya shingo pia kumchoma kisu kifuani  juu  ya  titi  la  kushoto.

Alisema  kuwa chanzo cha mauaji hayo kimetokana na visa vilivyokuwepo baina ya hao marehemu na kuwa siku za nyuma  kijana  huyo  Thomasi  Tumuhirwe  aliwahi  kuhukumiwa kifungo  jela kufuatia kumuibia mama huyo  mbuzi  wake  watano.


Wananchi  walioongea  na  waandishi  wa  habari   katika  eneo  la  tukio  walisema  kijana  huyo  aliyeuwawa  kisha  kuchomwa moto  alikuwa  akijihusisha  na  vitendo  vya  wizi  wa  mali  kwenye  kijiji  hicho.

Rutambi  Mabati  alisema  kuwa   kutokana  na  tabia  hizo  wananchi   ndiyo  maana  waliamua  kuchukua  hatua  hiyo  ili kukomesha  wizi  na  vitendo  vya  kijana  huyo.

Marehemu  mama  Juliana  Tumuhirwe miaka (57), hakubahatika  kupata  mtoto  katika    maisha  yake kwani  majirani  walieleza  kuwa  alikuwa  akijufungua  watoto  kisha  wanafariki  dunia.

Polisi  wilayani Kyerwa limethibitisha kutokea kwa vifo hivyo ambapo mganga mfawidhi kutoka zahanati ya Kibingo Diana Tamba alifika eneo la tukio na kufanya uchunguzi wa kitababu kisha kuruhusu miili ya marehemu  kuzikwa.

Hata hivyo polisi wamewataka wananchi kutojichukulia sheria mkononi kuwa  hakuna mwananchi akiye juu ya sheria na kuwaasa kutii sheria bila shurti.

No comments:

Post a Comment