Friday, August 21, 2015

SHAHIDI WA NNE KATIKA KESI YA ALIYEKUWA MEYA WA MANISPAA YA BUKOBA AKAMILISHA USHAHIDI WAKE


SHAHIDI wa nne kwa upande wa utetezi, katika kesi ya aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Bukoba  Anatory Amani, amekamilisha kutoa ushahidi wake, baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Kagera kukubali kupokea CD mbili kama Vielelezo vya ushahidi wake.

Katika kesi hiyo ya Madai Namba mbili ya mwaka 2014,  Amani anaiomba  Mahakama hiyo imwamrishe Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba,  amfungulie  Ofisi  na kumtimizia haki zake kama Meya wa Manispaa hiyo.

Katika Vielelezo hivyo, Shahidi huyo ambaye ni Afisa Habari wa mkoa wa Kagera, Silyvestar Raphael alitoa CD mbili moja na Video na nyingine ya Sauti za mkutano ulioitishwa kwa ajili ya kusoma taarifa za ukaguzi maalumu uliofanywa na CAG- katika manispaa ya Bukoba.


Agost 10 mwaka huu, shahidi huyo hakumaliza kutoa ushahidi wake, baada ya kuibuka mabishano ya kisheria kati ya mawakili wa serikali wanaosimamia kesi hiyo na Wakili wa malalamikaji Aron Kabunga juu ya kupokea au kutopokea Vielelezo hiyo.

No comments:

Post a Comment