Thursday, August 20, 2015

WALIMU 47 WA AJIRA MPYA WAINGIA MITINI

WALIMU 47 wa shule za sekondari kati ya 133,  waliokuwa wamepangwa na serikali kwenye ajira mpya mwaka huu, kwenye halmashauri ya wilaya ya Bukoba mkoani Kagera bado hawajaripoti  katika Vituo vyao vya kazi.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Graides Dyamvunye alisema kuwa mpaka sasa ni walimu 86, ambao tayari  wameripoti kwenye Vituo vyao vya kazi wakiendelea na shughuli zao za ufundishaji.

Alisema tarehe ya mwisho ya kuripoti kwa walimu hao, katika vituo vyao vya kazi ilikuwa Juni 9 mwaka huu na kusisitiza kuwa matumaini ya walimu hao kuripoti ni mdogo kutokana na muda wa kuripoti kuisha bila kuwepo kwa taarifa zao.

No comments:

Post a Comment