Na Juhudi
Felix-KYERWA
Mtu mmoja
mkazi wa Kitongoji cha
Kishanda B Kijiji cha Kyerwa
Kata ya Kyerwa
wilayani Kyerwa mkoani
Kagera amekutwa amejinyonga nyumbani
kwake na kuacha
ujumbe unaelezea sababu za kujinyonga
kwake kuwa ni
kukataliwa kwa mchumba wake
waliokuwa wanatarajia kufunga
ndoa Agosti 28 mwaka
huu.
Akithibitisha tukio
hilo jana mwenyekiti
wa kitongoji hicho Ibrahimu Paschal alisema kuwa
aliyejinyonga ni Sabinus Gabriel
miaka (30) na alitumia kamba ya
katani aliyoifunga kwenye
dari ya nyumba
yake.
Alisema
marehemu aliacha ujumbe aliouandika ukielezea
sababu zilizopelekea
kuchukua uamuzi huo
wa kujiua kuwa
ulitokana na kukataliwa
na binti aliyekuwa
anamchumbia na taratibu
zilikuwa zimeishakamilika na
mchumba wake huyo
kubadili maamuzi ghafla
na kumweleza hamtaki
tena kwasababu amempata
mwingine.
Aliyejinyonga
alitarajia kufunga ndoa
Agosti 28 mwaka huu
ambapo wana ndugu
walieleza kuwa taratibu
za kutoa mahali
zilikuwa zimeishafuatwa ambapo
Jumatatu ya Agosti 17
mwaka huu baadhi
ya vitu vilipelekwa
kwa wazazi wake
na binti.
Mwenyekiti
huyo alisema kuwa
tukio hilo la
watu kujinyonga katika
kijiji hicho ni
la pili ndani
ya wiki mbili
kwani kuna baba
mmoja alijinyonga baada ya
mke wake kuondoka
na kurudi kwa wazazi wake
huku akihaidi kutorudi kwake
na ndoa yao
haipo tena kutokana
na kile kilichodaiwa
ni kuwepo migogoro
ya muda mrefu ndani
ya familia hiyo.
Aidha Mzazi
wa marehemu Gabriel Rubinduka alieleza kusikitishwa na tukio la kifo
cha mtoto wake ambaye walitarajia kumfanyia sherehe kama walivyokuwa wameazimia kutokana na
maandalizi yaliyokuwa yamefanyika katika familia yao.
“Ni majonzi
makubwa kweli familia
tulishajiandaa kumwandalia sherehe
kubwa lakini hili lililomtokea sijui
kama ni mipango
ya Mungu ila
yote tunamwachia aliyetuumba
na kilichobakia ni
kuendelea kumwombea pumziko
la Amani”Alisema Gabriel
Binti
aliyekuwa anachumbiwa Jovitha
Novath alipofuatwa na
waandishi wa habari kuelezea
mkasa huo kama
ujumbe ulioachwa na
marehemu kama una
ukweli ndani yake
hakuwa tayari kuzungumzia
tukio hilo.
Kwa
upande wake Novath
Kalekona ambaye ni
mzazi wa binti
aliyekuwa anachumbiwa alikiri
kuwa ni kweli
binti yake kuchumbiwa
na huyo aliyejinyonga
na kusema kuwa
ni kweli baadhi ya mali
alikwishapokea kutoka kwa
wazazi wake na
marehemu.
“Ni
kweli wazazi wa
marehemu walileta mali
ambazo kwa makubaliano
ambayo ni taratibu
ambazo ni utamaduni
wetu lazima kuzitimiza
na walikuwa kwangu
jumatatu ya Agosti 17
mwaka huu lakini
hili la kujinyonga
limenishutua hata mimi na
hatukujua kama kuna hali
kama hiyo maana
walikuwa wakipendana kweli”Alisema
Kalekona
Jeshi la polisi
wilayani Kyerwa wameruhusu
mwili wa marehemu
kuzikwa baada ya
uchunguzi wa kitabibu
uliofanywa na mganga mfawidhi kutoka
Zahanati ya Kimuli Braisoni Katabaro.